Latest News
Sunday, 8 February 2015

Mwinyi:JKT inatakiwa kujitegemea katika kilimo.

Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa(jkt),Dk Hussein Mwinyi amevitaka vikosi vya Jkt  kujitegemea katika ufugaji na kilimo ili kutoa fulsa kwa vijana kutambua kwamba kilimo ndio kinachoweza kuwatoa katika umasikini.

Hayo aliyasema jana mkoani Dodoma wakati wa  ziara yake yakujionea shughuli zinazofanywa na kikosi cha 834 kj kilichopo makutupora.

“Nimefurahishwa na shamba la ufuta,pamoja na mavuno   mazuri yatachangia kuwajenga vijana kisaikologi kuhusu umaana wa kufanya kazi za kilimo kwa utalaama,”alisema Waziri Mwinyi.

Mwinyi alisema jkt inapojitegemea itawezesha  kusonga mbele na kwamba wanachofanya wao ni kutafuta mazao ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ili kua na uhakika na mapato ya shughuli za kilimo na nyingine za vikosi nya jeshi.

“Tunaendelea kutafuta soko kwa ajili ya bidhaa zetu tunazozalisha wakati mwengine wafanyabiashara wajanja wanabadilisha bei hasa pale mazao yanapokua tayari,”aliongeza Mwinyi.

Pia aliongeza kuwa serikali itaendelea na kazi ya kuboresha makazi ya askari kwa kuwajengea nyumba bora.

Alisema pamoja na wizara  kupatiwa fedha kidogo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo lakini wataendelea kuomba hazina ili waweze kuhakikisha askari wanaishi katika nyumba zenye ubora ili kwenda na dunia ya tatu ya sayansi na teknologia.

“Nimeona  shughuli mnazofanya pamoja na hayo ni lazima tuhakikishe mnakua na makazi bora ya kuishi,tumeanza na kimbiji kwa kujenga maghorofa manne,sasa tunaendelea na sehemu nyingine,”alisema Mwinyi


Mwinyi alisema serikali imejipanga kuweka mazingira mazuri ya askali wote Tanzania kwa mtu anapolala pazuri inamsaidia kufikilia kwa upana zaidi.
                  By Arapha Hussein



  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Mwinyi:JKT inatakiwa kujitegemea katika kilimo. Rating: 5 Reviewed By: NEWS EXTRAL