Pochi ni muhimu
sana katika maisha ya mwanamke yeyote.Pochi utumika kila eneo la maisha kuanzia nyumbani
,kazini kanisani,n.k
POCHI SAIZI YA KATI.
POCHI YA SAIZI YA KUBWA
POCHI YA MKONONI[clutch/Purse]
WALETI.
Pochi zipo za aina mbalimbali kwa matumizi mbalimbali.Pochi
uongeza umaridadi katika muonekano wa mwanamke hivyo ni muhimu kuangalia ubebeji
wa pochi kulingana na mahali,tukio na hata ikiwezekena mavazi.
POCHI SAIZI YA KATI.
Pochi hii utumika katika shuguli mbalimbali za kila siku
inafaa iwe na rangi itakayokuwezesha kuivaa na nguo nyingi iwezekanavyo,mfano rangi nyeusi,dark
brown,audark grey.Pochi hii aifai iwe na vikorombwezo vingi ,iwe tu plaini
yenye muundo wa kuvutia na uwezo wa kubeba vitu muhimu vya kila siku kama
waeti,simu ,diary,na vitu vingine vidogodogo.Pochi hii unaweza kwenda nayo
kazini,kanisani,mkutanoni,n.k.
POCHI YA SAIZI YA KUBWA
Inaweza kuwa ya ngozi au vinginevyo,kwa rangi yoyote
unayoipenda na kwa aina yoyote ile.Pochi
hii utatumia kwenda nayo shopping
au matembezeni yoyote ambayo unajua utahitaji kuweka vitu vingi kwenye pochi
,kwa wale wenye watoto wadogo pochi hii inafaa sana maana itakuwezesha kubeba
mahitaji yote ya mtoto kama diapers,maziwa,juice,nguo,nepi n.k.
POCHI YA MKONONI[clutch/Purse]
Pochi hii maalumu hasa unapotok usiku kwenda kwenye sherehe
au chakula cha usiku.Zipo za aina na rangi tofauti na inapendeza zaidi kama
ukimechi na rangi ya viatu au herein.Ni ochi ya kushiks mkononi na itakuwa na
uwezo wa kuweka vitu vidogodogo kama simu,lipshiner,lipstick.
WALETI.
Hii ni pochi ndogo ambayo mara nyingi huwekwa ndani ya pochi
kubwa na hubeba fedha,kadi mbalimbali,risiti na hata simi.Waleti zipo za
aina tofauti huweza pia kutumika yenyewe
pale unapokuwa unaenda mahali ambapo huitaji kubeba vitu vingi zaidi vinavyokaa
ndani ya wallet.
POSTED BY NAOMI KIPANGULA.
Instagram;African quuen.
Facebook;NAOMI KIPANGULA.
0 comments:
Post a Comment