TAKWIMU za hivi karibuni za Hospitali ya Ocean Road,Dar es
salaamzinaonesha wagonjwa wa sarataniwameongezeka hivi sasa ukilinganisha na
ilivyo kuwa miaka ya 90.Hivi karibuni ugonjwa huu umegusa hadi maisha ya
kiongozi wetu Mh,Raisi JakayaKikwete ambaye amerudi wiki chache zilizo pita
akitokea Hospitali ya Johns Hopkins ya nchini Marekani kwa upasuaji wa kuondoa
Saratani ya tezi dume(prostate cancer)
Pamoja na kuwepo sababu zingine zinazo weza
kusababishasaratani mbalimbali,taarifa iliyo tolewa mwaka 2006 na Hospitali
hiyo ya Johns Hopkins,ilihusisha matumizi ya vyombo vya plastiki kuandalia
vyakula na ugonjwa wa saratani,hasa saratani ya matiti.
Katika taarifa hiyo Hopkins waliorodhesha mambo matatu ya
matumizi ya vifaa vya plastiki ambayo yamegundulika kuababisha saratani ya matiti na kuwataka
watu wajiepushe na tabia hizo,ambazo ni
MOJA; usiweke chakula chako kwenye kontena au chombo cha
pastiki na kisha kupasha moto kwa kutumia microwave au maji moto kwa ajili ya
kula,
PILI; Usiweke maji kwenye chupa ya plastikina kisha
kuyagandisha kwa kutumia friza,kwa kifupi usitumie chupa ya plastiki kwa
kugandisha maji ya kunywa na,
TATU; Usiweke chakul chako kwenye mfuko wa plastiki na kisha
kupasha moto kwa njia nyingine ama microwave,ufungaji wa chakula kama vile
ufungaji chipsi za moto na kunywea chai
ya moto kwenye vikombe vya plastiki navyo ni hatari huweza sababisha ugonjwa wa
saratani,
Wataalamu wanashauri kutumia vyomb o vya udongo,chuma na
hata miti kama vile ungo ambavyo havina madhara kwa bindamu,
Tahadhari hiyo imetolewa baada ya wataalamu kugundua kifaa
cha plastiki kinapo pata joto au baridi kali hutoa kemikali ijulikanayo kama
DIOXIN amabayo imegundulika kusababisha saratani.
Kwakuwa ugonjwa wa saratani umeonekana kukua kwa kasi na
iddi ya wagonjwa wa saratani kuongezeka ,Watanzania hatuna budi kuangalia upya
staili ya maisha tunayo ishi n unapotolewa ushauri kama huu hatuna budi
kuuzingatia ili kujiepusha na gonjwa hili hatari.
0 comments:
Post a Comment