Latest News
Monday, 2 February 2015

BREAKING NEWS:Bondia Francis Cheka amehukumiwa kwenda jela.

Bondia Francis Cheka leo February 2 2015 amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na faini ya Milioni moja laki sita kwa kosa la kumpiga mmoja kati ya wafanyakazi wake kwenye bar yake iliyopo Morogoro.
cheka
Muda mfupi uliopita Francis Cheka ameongea na millardayo.com na kusema ndio alikua anajiandaa kuachia simu yake na vitu vingine muhimu ili achukue karandinga kuelekea gerezani ambapo namnukuu akisema ‘imeshakua hivi tayari ila hamna noma, niko na wanangu wengine wamepigwa miaka 10 nitakua nao fresh tu ila hamna noma ni miaka mitatu tu mimi’
Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Said Msuya ambapo baada ya hayo upande wa Francis Cheka unasemekana kujiandaa kukata rufaa.



  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: BREAKING NEWS:Bondia Francis Cheka amehukumiwa kwenda jela. Rating: 5 Reviewed By: NEWS EXTRAL