Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC), Nakuala Senzia (wa kwanza kulia), akizungumza
wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Dunia ya mwaka 2015 kuhusu uwekezaji
mara tu baada ya kuizindua kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es
Salaam jana. Pembeni yake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dk.
Florence Turuka (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC), Prof. Lucian Msambichaka (Katikati) na Mjumbe
wa kamati ya Bodi ya TIC, Dr Frances Shao.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Dk. Florence Turuka (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji
nchini (TIC), Prof. Lucian Msambichaka kwa pamoja wakizindua ripoti ya
Dunia ya mwaka 2015 kuhusu uwekezaji kwenye hafla fupi iliyofanyika
jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Dk. Florence Turuka (wa pili kulia) akionyesha ripoti ya Dunia ya mwaka
2015 kuhusu uwekezaji mara tu baada ya kuizindua kwenye hafla fupi
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Nakuala Senzia (wa
kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Prof. Lucian Msambichaka (wa
pili kushoto) na Mjumbe wa kamati ya Bodi ya TIC, Dr Frances Shao.
Baadhi ya wageni waalikwa na
wafanyakazi wa TIC waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa ripoti ya
Dunia ya mwaka 2015 kuhusu uwekezaji iliyofanyika jijini Dar es Salaam
jana wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali kuhusu uwekezaji
zilizoambatana na uzinduzi huo.
…………………………………….
Na Mwandishi watu
Tanzania imefanikiwa kukuza
uwekezaji wa nje wa moja kwa moja (FDI) kwa asilimia 14.5 ongezeko
linaloelezwa kuchangiwa na uvumbuzi wa gesi hapa nchini.
Kwa mujibu wa ripoti ya Dunia ya
mwaka 2015 kuhusu uwekezaji iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam,
ongezeko hilo linaifanya Tanzania iendelee kuwa kinara kwenye aina hiyo
ya uwekezaji dhidi ya mataifa mengine yanayounda Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Hata hivyo ripoti hiyo imebainisha
kuwa dunia kwa ujumla imeporomoka kwenye aina hiyo ya uwekezaji kwa
asilimia 16 hadi kufikia kiasi cha sh. Trilioni 1.2 katika kipindi cha
mwaka 2014 hali iliyosababishwa na mdororo wa uchumi wa dunia sambamba
ukosefu wa sera rafiki katika uwekezaji miongoni mwa mataifa mengi
duniani.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa
Uwekezaji na Uwezeshaji, Muhandisi Christopher Chiza katika hafla ya
uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Flolence Turuka alisema kiasi cha
uwekezaji huo hapa nchini kimekuwa zaidi kwa mwaka 2014.
Alisema katika mwaka 2014 taifa
lilifanikiwa kuvutia uwekezaji wenye thamani ya sh. Milioni 2,142
ikilinganishwa na kiasi cha sh. Milioni 2,131 mnamo mwaka 2013.
“Kiasi hiki ni kikubwa zaidi
ikilinganishwa na kiwango cha chini zaidi cha dola 640 kati ya mwaka
2005-2007 (kabla ya mgogoro wa uchumi). Mafanikio haya yanatokana na
uvumbuzi wa gesi hapa nchini na hivyo kuifanya nchi yetu kuendelea kuwa
kinara kwenye aina hii ya uwekezaji ililinagnishwa na nchi nyingine
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,’’ alisema.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo Uganda
inashika nafasi ya pili katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuvutia
uwekezaji wenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni 1.147 ikifuatiwa
na Kenya iliyovutia Dola za Kimarekani milioni 989.
Nchi za Rwanda na Burundi
zimeshika nafasi ya nne nay a tano kwa kuvutia uwekezaji wa thamani ya
dola za Kimarekani milioni 268 kwa Rwanda huku Burundi ikifanikiwa
kuvutia aina hiyo ya uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani
milioni 32.
Zaidi ripoti hiyo imebainisha kuwa
Afrika Kusini ndio inaoongoza barani Afrika kwa aina hiyo ya uwekezaji
kwa mwaka 2014 hukunafasi kama hiyo ikishikiliwa na China katika ngazi
ya kidunia, ikifuatiwa na Hong Kong huku Marekani ikitajwa kushika
nafasi ya tatu.
Zaidi ripoti hiyo imebainisha kuwa
katika mataifa kumi yanayofanya vizuri kwenye aina hiyo ya uwekezaji,
nusu yanatoka kwenye kundi la mataifa yanayoendelea yakiwemo Brazil,
Hong Kong, India na Singapore.
Katika mazingira haya kuna haja ya
kuimarisha sera za uwekezaji za kimataifa ikiwa ni pamoja na
Makubaliano ya uwekezaji ya kimataifa (IIA) huku pia suala la kodi za
kimataifa likipewa kipaumbele,’’ alisema.
Katika hotuba yake ya ufunguzi,
Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji hapa nchini (TIC),Prof. Lucian
Msambichaka pamoja na mambo mengine alikipongeza kituo hicho kwa
jitihada zake katika kuvutia uwekezaji hapa nchini sambamba na kupunguza
vikwazo katika uwekezaji huo.
0 comments:
Post a Comment