Latest News
Tuesday, 30 June 2015

mastaa wenye pesa mwaka huu wa 2015


Forbes Magazine jarida la Marekani limeachia orodha ya wasanii 100 wenye pesa zaidi kwa mwaka huu wa 2015, na kwenye orodha hiyo utakutana na watu kama Katy Perry, Beyonce, Kim Kadarshian, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao, Taylor Swift na wengine kibao so unaweza ukavuta picha nani kampiku nani kwenye uwezo wa kifedha mwaka huu.
Staa anayeshika kijiti kwenye orodha ya mwaka huu ni Floyd “Money” Mayweatherakiwa na thamani ya millioni $300 , Manny Pacquiao kwenye nafasi ya pili akiwa na thamani ya $160 millionKaty Perry akishika nafasi ya 3 akiwa na thamani ya millioni $130.
FLYOD
Gari jipya la Floyd Mayweather “Koenigsegg CCXR Trevita” yako matatu tu duniani, na hili ni moja wapo.
Kuonyesha uwezo wake wa kifedha, Floyd “Money” Mayweather kaamua kununua gari jipya, gari lenye thamani ya millioni $4.8, aina ya Koenigsegg CCXR Trevita gari ambalo kwenye rekodi ya dunia yapo matatu tu, na sasa akiwa mmoja kati ya watatu wanaolimiliki gari hilo!
FLOYD 2
Hii ni picha inaonyesha jumla ya magari na ndege alionayo Floyd Mayweather. Kila gari limewekwa thamani yake.
Hapa chini nimekusogezea orodha ya mastaa kumi tu kutoka kwenye list ya Forbes 100 Richest Celebrities 2015. 
1. Floyd Mayweather ($300 million)
2. Manny Pacquiao ($160 million)
3. Katy Perry ($130 million)
4. One Direction ($130 million)
5. Howard Stern ($95 million)
6. Garth Brooks ($90 million)
7. James Patterson ($89 million)
8. Robert Downey Jr. ($80 million)
9. Taylor Swift ($80 million)
10. Cristiano Ronaldo ($79.5 million)


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: mastaa wenye pesa mwaka huu wa 2015 Rating: 5 Reviewed By: Bongo Trending