Latest News
Sunday, 8 February 2015

Dalili, Isharaza mjamzito kujifungua


Tuliona kuwa kipindi cha kujifunga hutabiriwa lakini siku rasmi mara nyingi haitabiriki. Wengi hufikiria kuwa dalili ya kwanza ya kutaka kujifungua ni kupasuka kwa chupa. Hii si sahihi, chupa inaweza isipasuke hadi hadi hatua za mwisho.

Katika makala ya NYAKATI TOFAUTI ZA KUJIFUNGUA tuliangalia kuhusu umri wa mimba ambao kiumbe kilichoko tumboni mwa mama kilichoka basi huhesabiwa kama mama amejifungua.


Mara nyingine hulazimika kuipasua ili kuharakisha hatua za kujifungua. Dalili za wazi kabisa za kujifungua ni ile ya kuwepo kwa uchungu ambazo asili yake ni katika mfuko wa uzazi.

Uchungu huu ni ule ambao una mpangilio na ongezeko kwa muda maalumu ambao huenda sambamba na kusinyaa na kufunguka kwa shingo ya mfuko wa uzazi.

Dalili ya kufunguka huku huwa ni kutokwa kwa ute mithili ya mlenda uliochanyika na damu.  Ni lazima kwa mjamzito anapopata dalili hizi kati ya wiki 24 na 42 kuripoti katika kituo cha afya ili achunguzwe.
Hata kama hali hii ikitokea kabla ya muda huo, ni lazima kuwahi kwemye kituo cha afya kwani ni dalili ya mimba kutoka.
Dalili nyingine inayoashiria kujifungua ni kushuka kwa mtoto kwenye nyonga katika mwelekeo wa kutoka kupitia njia ya uzazi. Jambo hili lazima liwepo baada ya uchungu na kufunguka kwa njia.

SOMA PIA : MAZOEZI KWA WANAWAKE WALIOJIFUNGUA KWA UPASUAJI

Kama uchungu na kufunguka kwa njia vinakuwapo lakini mtoto hashuki wala husogea kwenye njia za kutokea, basi lazima huchukua hatua za kujua sababu.  Kukwama huku kunaweza kuletwa na sababu nyingi. Moja ya sababu hizo ni kutokuwapo kwa uwiano mzuri kati ya ukubwa wa kichwa cha mtoto na ukubwa wa nyonga ya mama.

Kwa kawaida kama mjamzito anaendelea vizuri na hakuna vikwazo, huchukua wastani wa saa nane mpaka 12 kujifungua. Muda huu huwa zaidi ya hapo kama mtoto amekwama kwa sababu yoyote ile.

SOMA MAKALA HII : UKWELI JUU YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA

Mtoto aliyekwama huwa katika hatari ya kupoteza maisha kama hatua za haraka hazita chukuliwa. Inapopaswa kueleweka kwamba kitendo cha kujifungua ni hatarishi wakati wote na hivyo uangalizi na ufuatiliaji wa kila hatua muhimu.
Wakati mwingine dharura inaweza kutokea wakati wowote na kulazimika kufanywa uamzi ambao hapo awali hakufikiriwa.





  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Dalili, Isharaza mjamzito kujifungua Rating: 5 Reviewed By: NEWS EXTRAL