Latest News
Friday, 26 June 2015

KAPUMZIKE KWA AMANI MPIGANAJI MWENZETU EDSON KAMUKARA.

Mhariri  wa Mwana Halisi Online, Edson Kamukara (pichani), amefariki Dunia kwa ajali ya moto nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam leo hii majira ya saa moja kasorobo jioni, baada ya kulipukiwa na jiko la gesi, habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Polisi wameuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuhifadhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa kifo chake.
 

Ofisa Uhusiano wa NMB, Viccent Mnyanyika akimkabidhi zawadi marehemu Edson Kamukara wakati wa uhai wake kwenye wa utoaji wa tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) zilizofanyika Aprili 24 mwaka huu.

Hope news inaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake, marafiki na majirani katika msiba huu. Mola na aiweke mahala pema Roho ya Marehemu,
AMINA



  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: KAPUMZIKE KWA AMANI MPIGANAJI MWENZETU EDSON KAMUKARA. Rating: 5 Reviewed By: Anonymous