Latest News
Sunday, 8 February 2015

Mwakilishi wa darasa chuo kikuu cha iringa Lucy Seveline Ajiuzulu

Katika hali isiyo ya kawaida na katika mazingira ya kusikitisha na ya kutisha, kiongozi mmoja wa Kozi ya Uandishi wa Habari mwaka wa kwanza ngazi ya Shahada, katika Chuo Kikuu cha Iringa, Bi Lucy Severine amejiuzuru.
Akiongea mbele ya wanafunzi wenzake, kiongozi huyo mwenye kujiamini, akijaa bashasha alitangaza rasmi  nia yake ya kuachia madaraka. Katika kikao hicho kilichoitishwa na yeye mwenyewe, alisema "Nawashukuruni sana ndugu zangu tumekuwa wote kwa muhula mzima, tumeshirikiana na kusaidiana kwa mengi, na katika mchana wa leo nimewaiteni hapa ili kuwaeleza nia yangu ya kuachia madaraka kwa sababu ninazozijua mimi na siwezi kuzisema."
Baada ya tangazo hilo kulitokea mazungumzo ya hapa na pale miongoni mwa wanadarasa hao na kufikia uamuzi wa kumchagua kiongozi mwingine ambaye atashika nafasi yake.
Ndugu Edwin K. Tongora aliteuliwa kuwa msimamizi wa uchaguzi huo, na majina ya watu wawili yalipendekezwa, ambao ni Zaina Malogo, na Judith Mkomo. Baada ya zoezi la upigwaji kura, Bi Judith Mkomo alimshinda Bi Zaina Malogo kwa kupata kura 21 dhidi ya 19, hivyo msimamizi wa uchaguzi kumtangaza Judith kuwa kiongozi mpya wa darasa hilo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Mwakilishi wa darasa chuo kikuu cha iringa Lucy Seveline Ajiuzulu Rating: 5 Reviewed By: NEWS EXTRAL